Skip to main content

SERIKALI YA MAREKANI YATOA MAGARI MATATU KWA AJILI YA KUPAMBANA NA UJANGILI

Serikali ya Marekani imetoa msaada wa magari matatu aina ya Land Cruiser kwa TAWA kwa ajili ya kusaidia jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na ujangili . Gari hizo zimekabidhiwa na balozi wa Marekani hapa nchini Dkt  Inmi Patterson kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali Mstaafu Khamis Semfuko ili kusaidia mapori ya Akiba Rungwa/Muhesi na Kizigo.