Skip to main content

TANGAZO LA MNADA WA MENO YA VIBOKO

TANGAZO LA MNADA WA MENO YA VIBOKO KWA WAFANYABIASHARA WALIOPEWA LESENI ZA NYARA DARAJA LA 1 MWAKA 2017

 

Wafanyabiashara wa biashara ya nyara waliopewa leseni ya Nyara Daraja la 1 ‘Meno ya Viboko’ mwaka 2017 wanatangaziwa kwamba meno ya viboko vipande 12,467 yenye uzito wa Kg 3,580.29 yatauzwa katika mnada wa hadhara chini ya usimamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango tarehe 29 Januari, 2018.

Mnada utafanyika katika Jengo la Mpingo, Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam zilipokuwa Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utaliii (Ivory room). Meno hayo yanaweza kukaguliwa tarehe 25 na 26 Januari, 2018 kuanzia nne asubuhi hadi saa tisa na nusu jioni.

 

MASHARTI YA MNADA

1.    Wafanyabiashara watakaoshiriki mnada ni wale waliopewa leseni ya nyara daraja la 1 mwaka 2017,

2.    Wanunuzi wanatakiwa kulipa asilimia ishirini na tano (25%) ya bei papo hapo na asilimia sabini na tano (75%) italipwa yote katika muda wa siku kumi na nne (14) baada ya mnada;

3.    Mtu yeyote atakayekuwa ametamka bei ya juu, kisha akashindwa kulipa asilimia ishirini na tano (25%) ya bei aliyotamka, atachukuliwa kuwa ni mwenye kutaka kuvuruga mnada na hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake;

4.    Meno yatauzwa kwa wastani wa uzito wa nusu kilo (0.5kg) bila kugawanywa au kuchambuliwa wakati wa mnada; na

5.    Wanunuzi wataruhusiwa kuondosha bidhaa kwenye eneo la mnada baada ya kulipia ada na kodi husika kikamilifu na kupewa hati ya kumiliki nyara,

6.    Mnada utafanyika kuanzia saa nne asubuhi.

 

MKURUGENZI MKUU

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA-TAWA